post image
Ibada ya kubariki Wachungaji watano na Wadiakoni watatu kuweka Nadhiri

Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara ameongoza ibada ya Kubariki ili kuwaingiza katika huduma Wachungaji watano pamoja na Wadiakoni watatu walioweka Nadhiri ya kuwa Sista wa Maisha, watakaoifanya kazi ya Mungu katika dayosisi hiyo.

Ibada hiyo imefanyika Tarehe 15/12/2024 katika Kanisa kuu KKKT/DKMG-Bukoba na kuhudhuriwa na maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali viongozi wa dini pamoja na waumini wa Kanisa hilo.

Wachungaji hao waliobarikiwa ni Mchg. Avitus Momo Gration, Mchg. Damian Mwemezi Kisimbe, Mchg. Dickson Rweyemamu Pius, Mchg. Elisa Mtegeki Ezra pamoja na Mchg.Pius Kaizilege Philbert.

Kwa upande wa Masista walioweka Nadhiri ya kuwa Sista wa Maisha ni Sr. Adventina Kokuberwa Kyamanywa , Sr. Erica Kokwenda Mbekenga na Sr. Jerda Ebyalipima Shumuni.

Mchungaji wa jimbo la Kati Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mchg. Justinian Kato wakati akihubiri katika ibada hiyo amewataka Wadiakoni walioweka Nadhiri zao kufanya kazi ya Mungu kwa kufuata misingi iliyopo katika Katiba ya Dayosisi ya Kaskazini Magharibi toleo la mwaka 2008

Aidha amewapongeza Wachungaji walioingizwa Katika huduma ya Uchungaji na kuwataka kufanya kazi kwa kujituma huku wakizingatia nadhiri waliyoiweka mbele ya Madhabahu wakati wa kubarikiwa.

Hata hivyo amewataka Wachungaji hao kutumia vizuri Mamlaka waliyopewa kwa kuwabariki watu ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kukabiriana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika utumishi wao.

post
post
post
post