DKMG imepokea wachungaji wamisionari wawili vijana kutoka Nchini Indonesia
Wageni ni Baraka!
Tunamshukuru Mungu sana, DKMG imepokea wachungaji wamisionari wawili vijana (Me na Ke) kutoka kwenye Kanisa la Kiprotestant la Indonesia (HKBP) ambao watatoa huduma kwenye DKMG kwa miaka 3 (renewable).
Kanisa la Indonesia katika kuadhimisha miaka 125 ya Injili limeamua kutuma wachungaji wamisionari kwenye makanisa rafiki hapa Afrika.
DKMG imepokea wachungaji hao ambao wameambatana na Askofu wao Ephorus Rt. Rev. Dr. Robinson Butarbutar pampja na Mchg Dkt. Ernest Kadiva ambaye ni kiongozi wa shirika la kitume la UEM kwenye ukanda wa Afrika.
Wana DKMG wakiongozwa na Mheshimiwa Dean Prof. Josephat Rweyemamu wamewapokea kwenye uwanja wa ndege na kuwafikisha ELCT Bukoba Hotel. Akitoa neno la makaribisho Mhe Dean amesema miaka mingi tulizoea kupokea wamisionari kutoka Ulaya na Amerika ni furaha iliyoje kuwapokea kutoka Mashariki ya mbali (South East Asia). Amewakaribisha kwa furaha na kuwatakia ufanisi katika utume.
Naye Baba Askofu Robinson Butarbutar ameshukuru sana mapokezi na amemshukuru Baba Askofu Dkt. A. Keshomshahara ambaye ni kiongozi mkuu wa shirika la UEM duniani kwa kukubali mawazo ya kanisa la Indonesia kutuma wamisionari kwenye marafiki waliopo Afrika.
Naye Mchg Dkt Kadiva ameshukuru mapokezi na kuomba DKMG iwatunze vizuri wamisionari hao,
Kwaya ya Wanawake na Kwaya ya Tarumbeta kutoka Kanisa kuu zimenogesha mapokezi hayo.
Tunawashukuru wote waliohusika katika kuhakikisha mapokezi hayo yanafanyika kwa ufanisi
Wamisionari hao watasimikwa rasmi hudumani jumapili tarehe 7/7/2024 na Baba Askofu Keshomshshara akishirikiana na Baba Askofu Robinson Butarbutar.
Tunawatakia wamisionari wetu utume mwema.