post image
Ugeni kutoka DANIDA

Tarehe 20/4/2024 Dayosisi (DKMG) ilipokea ugeni kutoka DANIDA Ofisi ya nchi pamoja na makao makuu (Denmark).

Ugeni huo ulilenga kutathmini shughuli za maendeleo ambazo zimewahi kufanyika kwa ubia (partnership) kwa njia ya moja kwa moja au kupitia serikali. Pia ulilenga kuona FBO ikiwemo DKMG zinaweza kutumia approach ipi kufikisha maendeleo kwenye jamii ukizingatia kuwa Ubalozi wa Denmark utarudishwa Tanzania, tofauti na ilivyokuwa imeamuriwa huko nyuma.

Mwaka 2022 na 2023 binafsi nilibahatika kushiriki na kuwa mmojawapo wa wana jopo lililokutana na Waziri wa Mambo ya nje wa Denmark, tukiwa Hellerup Copenhagen,  tukiomba Ubarozi wa Denmark usifungwe maana partnership yetu na watu wa Denmark, kupitia KKKT, hasa katika kuwaletea wananchi wetu maendeleo bado ni kubwa.

Mazungumzo na wageni waliotufikia jumamosi yalikuwa mazuri. Danida walifurahi na walishangaa kuona magari waliyoyatoa kwa njia ya Program ya PHC (Primary Health Care) miaka ya 2000’s bado yapo yanafanya kazi za kanisa.

Tunamshukuru Mungu kwa ugeni huo, tunatarajia matunda yatakayoinufaisha jamii huko mbele.

post
post