post image
KKKT Kanisa kuu Bukoba

07.07.2024 KKKT Kanisa kuu Bukoba. Wachungaji 2 kutoka Indonesia Kanisa la BATAK HKBP wametumwa na kanisa hilo kutumika DKMG Bukoba kwa miaka 3 inayoweza kuhuishwa upya.

Wametumwa jumla wachungaji 12 Barani Afrika. Hii ni kuadhimisha miaka 125 ya uinjilishwaji wa Indonesia wakaona nao washiriki uinjilishaji duniani.

Mmoja atahudumu kanisa kuu na idara ya vijana na mwingine Usharikani Ibura na kufundisha Muziki Ntoma.

Wameingizwa kazini na kukabidhiwa kwa Dayosisi na Ephorus Dr. Robin Butarbuta mkuu wa kanisa hilo nchini Indonesia ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa UEM Asia. 

Mungu abariki huduma yao, Amina.

post
post
post
post
post
post