post image
Semina ya Watendakazi wa Huduma ya Mtoto kwa ubia na Compasion International Tanzania...

20-21 Februari 2024 KKKT Kashura Women Center. Semina ya Watendakazi wa Huduma ya Mtoto kwa ubia na Compasion International Tanzania. Mada zilihusu maboresho ya utendaji kazi katika vituo vya huduma ya mtoto ndani ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Bukoba. Watendakazi zaidi ya 40 kutoka vituo 10 vya huduma ya mtoto wamehudhuria wakijumuisha wachungaji katika vituo husika, waratibu, wahasibu na maafisa jamii pamoja na mratibu wa shughuli za diakonia katika dayosisi. Vituo hivi husaidia watoto kupata elimu ya kujitambua, dini, msaada wa karo hadi chuo kikuu, tiba/Bima ya afya, huduma ya maji katika baadhi ya maeneo kuhudumia wanajamii, elimu ya kujitegemea, chakula siku ya masomo Jumamosi na mahitaji kadhaa kwa ajili ya  shule.Watoto zaidi ya 2.000 wanafikiwa na huduma hii katika vituo 10 ndani ya dayosisi. Mungu azidi kubariki yote yawe mema. Amina.

post
post
post
post
post
post
post
post