post image
Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani, Vatican

Baba Mtakatifu, Papa Francis amekutana na Uongozi wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani, Vatican

Uongozi wa walutheri uliongozwa na Raisi wa Fungamano hilo ambaye ni Askofu Henrik Stubkjae, Askofu wa Dayosisi ya Viborg kwenye Kanisa la Kilutheri nchini Denmark.

Wamekutana Vatican tarehe 20/6/2024 na kufanya mazungumzo kuhusu umuhimu wa umoja katika kumtangaza Kristo kwenye karne hii na zijazo.

Raisi wa FMKD amekumbusha safari ya mazungumzo yahusuyo umoja kati ya Kanisa Katholiki na Kanisa la Kilutheri, safari ambayo imetimiza miaka sitini hivi. Amekazia kuwa Umoja ni agizo la Bwana wetu Yesu Kristo. Amesema Walutheri wanaanza maandalizi ya Kuadhimisha Ungamo la Augusburg ifikapo 2030. Lengo la ungamo hilo lilikuwa ni kutunza na kuimarisha umoja wa Kanisa. Hakuna njia nyingine ya kutunza umoja wa kanisa isipokuwa kwa kuwa na uekumene wa vitendo.

Papa Francis akikazia amesema kiongozi wa umoja wa Kanisa ni Yesu Kristo mwenyewe. Akikazia umoja amekumbusha mkutano mkubwa wa Nicea uliotokeza imani ya mitume kwa mhutasari. Kazi kubwa katika uekumene ni kuhubiri Injili ya Kristo. Amekumbusha kuwa mwaka kesho tutatimiza miaka 25 tangu tusaini makubaliano yahusuyo fundisho muhimu la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu Kristo na akamaliza akisema makubaliano yetu hayo tuyaweke kwenye vitendo, na hii ni alama ya matumaini katika umoja wetu.

post