post image
Utambulisho wa watendakazi wapya DKMG

Katibu mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi ya Kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania Rev. Dr. Elmereck Kigembe ametambulisha watenda kazi wapya watakaohudumu katika vitengo mbalimbali ndani ya idara ya mipango, uchumi na maendeleo.

Watendakazi wapya waliotambulishwa ni pamoja na Bw. Danson Baselwa Kateme  ambaye ni Afisa masoko wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Kabla ya nafasi hiyo Bw. Kateme alikuwa Afisa mipango wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.

Pia amemtambulisha Bw. Davis Rweyemamu Dominick ambaye ni Afisa Mpango na mratibu wa Kitengo cha Mipango chini ya Idara ya Mipango,Uchumi na Uwekezaji ndani ya Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.

Aidha amemtambulisha Bw. Eliud Henry Kwelebela ambaye ni Afisa habari wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi na mratibu wa kitengo cha habari, kabla ya nafasi hiyo Bw. Eliud alikuwa mwandishi wa Habari na mhariri wa maudhui ya mtandaoni katika kituo cha habari cha Radio Karagwe FM sauti ya wananchi.

post Bw. Danson Baselwa Kateme, Afisa masoko DKMG
post Bw. Davis Rweyemamu Dominick, Afisa mipango DKMG
post Bw. Eliud Henry Kwelebela, Afisa Habari DKMG