post image
Ziara ya Bodi ya UEM

KKKT Dayosisi ya Karagwe, Kanisa Kuu, Lukajange, Ziara ya UEM wakati wa Bodi ya UEM Afrika. Salaam za UEM zimetolewa kwa waumini na pia Baba Askofu Dkt. Abednego Keshomshara amepata neema ya kuhubiri neno la Mungu kutoka Yoh 17:21 "wote wawe na umoja" huku kichwa cha Jumapili ya leo kikisema "Umoja wetu- Nguvu yetu'. Tumeipongeza dayosisi ya Karagwe kwa huduma nzuri ya uinjilishaji, Afya, Elimu, Diakonia, maendeleo na miradi mbalimbali inayogusa jamii ya watanzania wote bila kujali dini, kabila, itikadi, eneo, n.k. Wajumbe wa bodi ya UEM wamesambaa kutoa huduma katika mitaa ya Jimbo la Lukajange, Karagwe. Mungu azidi kubariki yote yawe mema. Amina.

post
post
post
post
post
post