post image
Tarehe 19/03/2024 DKMG ilitembelewa na Mkurugenzi wa Compassion Tanzania, Bibi Mary Lema...

Tarehe 19/03/2024 DKMG ilitembelewa na Mkurugenzi wa Compassion Tanzania, Bibi Mary Lema akiwa na ujumbe wake. Ziara hiyo ya Mkurugenzi hapa mkoani Kagera ililenga kutembelea makanisa wenza kuwa na mazungumzo na viongozi, kukagua shughuli kwenye vituo vya huduma ya mtoto pamoja na kuona maandalizi ya uendeshaji shughuli kupitia NGo baada ya Compassion yenyewe kusajiliwa kuwa NGo.

Mkurugenzi aliwasili saa moja na nusu asubuhi, mazungumzo yakifanyika. Baadaye alitambulishwa kwa Mkuu wa Mkoa. Baada ya chai ujumbe huo uliondoka kuelekea Minziro kwenye kituo cha huduma ya mtoto. Kesho asubuhi atatembelea kituo cha Huduma ya Mtoto pale Ibura.

Baba Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara,  alipata fursa ya kumshukuru Mkurugenzi kwa kuongeza vituo viwili zaidi na kukamilisha vituo kumi katika Dayosisi. Alishukuru pia kwa huduma ya mama na mtoto pamoja na kuongezewa watoto.

Mkurugenzi wa Compassion alieleza kuwa Compassion inaiona DKMG kuwa mshirika mwenza wa uhakika na mwenye mifumo wezeshi ya kuendeleza huduma ya mtoto.

Tunamshukuru sana Mungu kwa baraka ya ugeni huo.

post
post
post
post
post
post
post