post image
Ziara ya kwanza ya Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex G. Malasusa akimkaribisha Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (Lutheran World Federation “LWF”), Askofu Henrik Stubkjær ambaye amewasili nchini Tanzania hii leo akiwa na ujumbe wake tayari kwa kuanza ziara yake ya siku 3 ya kuitembelea Taasisi za KKKT.

Hii ni ziara yake kwanza kwa Rais huyo wa LWF Askofu Stubkjær mara baada ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu wa fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani uliofanyika Krakow, Poland mwezi Septemba, 2023.

Aidha, ziara hiyo itampa nafasi Rais huyo kujitambulisha kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambalo ni moja ya Makanisa wanachama wa Fungamano na atapata nafasi ya kuona maisha na kazi za Kanisa katika kuhubiri Injili, kumhudumia mwanadamu kwa ukamilifu wake kiroho, kiakili na kimwili.

post
post
post