post image
Timu hii imefanya kazi ya kuangalia...

PMT imeendelea kwenye hospitali ya Izimbya. Timu hii imefanya kazi ya kuangalia mifumo ya uendeshaji wa hospitali na kutoa ushauri kuhusu maboresho yanayotakiwa. Tunamshukuru Mungu zoezi limeanza vizuri na kukamilika vizuri. Viongozi wa hospitali wameipokea timu hii vizuri na kwa furaha. Hakika kazi inayoendelea kufanywa hapa Izimbya ni kubwa. Changamoto zipo ila kubwa ni ukosefu wa wodi ya private. Mabadiliko ya gharama za kitita cha BIMA ya Afya yaliyofanywa na serikali hivi karibuni nayo yataendelea kuathiri mapato ya hospitali.

Pamoja na mkataba wa CDH bado watendakazi wengi wako kwenye ajira ya kanisa. Haya matatu yataendelea kuathiri mapato ya hospitali. Watendakazi wote wana Bima ya afya na baadhi yao wamedhaminiwa mikopo kwenye benki ya CRDB.

Izimbya imeanza kupokea wagonjwa kutoka mkoani Geita kwa ajili ya huduma nzuri inayotolewa.

post
post
post
post
post