post image
Mazishi ya Marehemu Mwl. Ernest Lutabingwa aliyeaga dunia akiwa na miaka 97...

22.02.2024 Kijijini Kitendaguro, Bukoba Manispaa. Mazishi ya Marehemu Mwl. Ernest Lutabingwa aliyeaga dunia akiwa na miaka 97. Mazishi yamehudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa serikali akiwemo Mhe. Mbunge wa Bukoba Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Advocate Stephen Byabato na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima na wanajamii kutoka sehemu mbalimbali. Tangemu marehemu astaafu ualimu imepita miaka 43. Walikuwepo wanafumzi wake wengi akiwemo Dean Mstaafu ta Wilson Kyakajumba. Aliyetulisha neno ni Mch. Christopher Mbuga ambaye ameonesha mengi ya kujifunza kutoka kwa marehemu ikiwa ni pamoja na kuwa na imani thabiti, kumtanguliza Mungu, kuwa watu wa manufaa ktk kanisa na jamii na kutosumbua kamati za ulinzi na usalama ktk taifa. Mungu ampe marehemu E. Lutabingwa pumziko la amani na awafariji wafiwa wote daima.

 

post
post
post
post
post
post
post