post image
Siku ya furaha, nderemo na vifijo kwenye Shule ya Sekondari ya Bukoba Hope...

Tarehe 27/2/2024 ilikuwa siku ya furaha, nderemo na vifijo kwenye Shule ya Sekondari ya Bukoba Hope.

Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu/Idara ya Huduma za Jamii na Mratibu wa kitengo cha elimu tulihudhuria siku hiyo. Lengo la kufika huko lilikuwa ni mwaliko na ziara ya pongezi kwa shule kufanya vizuri sana katika mitihani ya taifa kidato cha pili na cha nne mwaka 2023

Ilikuwa ni furaha tupu ikiwa na matukio ya Show, ngoma, zawadi kwa wanafunzi washindi ambao wako kidato cha tatu sasa, zawadi kwa Walimu na watendakazi ambao sio walimu.

Tukio hilo pia lilikolezwa na tukio la shule kuzindua program ya E-learning ambapo vilizinduliwa vishikwambi  vyenye program ya masomo ya kidato cha kwanza ambavyo vitawawezesha wanafunzi kusoma topic hata bila mwalimu kwa kuona clips na vitabu vilivyo ndani ya vishikwambi hivyo. Program hii imehamasishwa na shirika la Education Opportunity lililoko Arusha.

Tunawapongeza Bukoba Hope kwa ushondi mnono na tunatia moyo kufanya vizuri zaidi

With God, we are strong, without God, we are weak.

post
post
post
post
post