post image
Timu hii imefanya kazi ya kuangalia...

PMT imeendelea Bukoba Town Health Centre. Timu hii imefanya kazi ya kuangalia mifumo ya uendeshaji wa kituo na kutoa ushauri kuhusu maboresho yanayotakiwa. Tunamshukuru Mungu zoezi limeanza vizuri na kukamilika vizuri. Viongozi wa kituo wameipokea timu hii vizuri na kwa furaha. Pamoja na ushindani unaotokana na kuwa na vituo vingine vya afya na Polyclinics, kazi inayoendelea kufanywa BTHC ni kubwa. Changamoto kubwa ni ufinyu wa kiwanja. Mabadiliko ya gharama za kitita yaliyofanywa na serikali hivi karibuni nayo yataendelea kuathiri mapato ya kituo.

Aidha kituo kimewekeza katika vipimo. Kuna Ultra sound digital mpya, Biochemistry machine, Hematological analyzer na mfumo thabiti wa kanzi data. Watendakazi wote wana Bima ya afya na baadhi yao wamedhaminiwa mikopo kwenye benki ya CRDB.

Msimu huu wa sikukuu inategemewa idadi ya wagonjwa ishuke na ipande sikukuu zikiisha. Staff ya BTHC inatuma salaam na kuwakaribisheni kituoni.

post
post
post
post
post